WATU wengi wamezoea kuona mwanaume anamuoa mtu ambaye si damu yake yaani waliozaliwa na baba na mama mmoja, hii ni kutokana na maandiko ya vitabu vya dini na jamii nyingi huamini katika hilo.
Lakini imekuwa tofauti sana na kijana mmoja raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Paulen Ziarirwa mwenye umri wa miaka 28 ambaye amemuoa dada yake wa damu aitwaye, Dorica Ziarirwa mwenye umri wa miaka 26.
Wanandoa hawa wamezaliwa kwenye familia moja kutoka kijiji cha Bunia ambacho kilitokea mgogoro wa kikabila na kusababisha watu kuuawa na wengine kukimbia makazi yao.
Ещё видео!