Mapema siku ya jana Rais wa Urusi Vladimir Putin alimkaribisha Waziri Mkuu wa India Narendra Modi ambaye yupo ziarani nchini Urusi kwa lengo la kuimarisha uhusiano kwenye maeno ya biashara ya nishati na uchumi kwa ujumla.
Mapokezi ya Modi yalikuwa ya aina yake, kwani licha ya Putin kumtembeza Modi kwenye makazi yake yaliyopo nje kidogo ya Moscow, wawili hao waliopoonana walisalimiana kwa bashasha na kukumbatiana kitu ambacho kilidhihirisha shauku ya mashirikiano baina ya wawili hao.
Hata hivyo wakati mapokezi hayo yakiendelea jijini Moscow, huko nchini Ukraine makombora ya Urusi yamelindima katika miji mbalimbali ikiwemo mji mkuu wa Kiev kupelekea vifo vya watu takribani 38 na wengine zaidi ya 190 wakijeruhiwa.
Unaweza kutufuatilia kupitia;
TWITTER: [ Ссылка ]
INSTAGRAM: [ Ссылка ]
FACEBOOK: [ Ссылка ]
TIKTOK: [ Ссылка ]_...
Au tembelea tovuti yetu: [ Ссылка ]
Je, una habari? wasiliana nasi kupitia Telegram/WhatsApp +255 753 815 105
The Chanzo Initiative, 2024 © All Rights Reserved.
![](https://i.ytimg.com/vi/UDzYqYt8wpo/maxresdefault.jpg)