Wafuasi wa CHADEMA waliofika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa ajili ya kufatilia mwenendo wa kesi ya ugaidi inayomkabili Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe wamekamatwa na Askari Polisi baada ya kuinua mabango na kupiga kelele kwamba "Mbowe sio Gaidi".
Kesi ya Mbowe inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba ambapo hata hivyo Mbowe hakufikishwa mahakamani bali kesi yake inaendeshwa kwa njia ya mtandao.
Mbowe ameshitakiwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu July 26, 2021 kwa mashtaka mawili ikiwemo la tuhuma za Ugaidi.
Ещё видео!